|
Makala hii au sehemu ya makala
hii inahitaji masahihisho kwa upande mmoja wa
zifuatazo:
·
msamiati, sarufi au
tahajia,
·
mpangilio
wa habari,
·
muundo
wa makala.
Ili kupata sababu angalia ukurasa wa
majadiliano.
|
Dunia uwanja wa fujo ni riwaya
iliyoandikwa na mwandishi Euphrase Kezilahabi mwaka wa 1975, ni
riwaya ambayo inasawili maisha ya wanadamu husani waishio Afrika Mashariki hasahasa katika nchi ya Tanzania.
“Dunia uwanja wa fujo” inaelezea jinsi
maisha yaliyopo duniani ni sawa sawa na fujo kwani kila mtu anayekuja duniani
huleta fujo zake na baadae kutoweka. Mwandishi E. Kezilahabi anaelezea katika
jamii kila mtu anakuja duniani kufanya fujo zake na kusababisha matatizo
mbalimbali katika jamii yake kama vile mauaji , ukabila, umalaya, uchawi,
ubakaji ulevi wa kupindukia nk. hivyo basi mwandishi anaamini kwamba katika
dunia kila mtu anakuja na fujo zake na kutoweka, mfano mhusika Tumaini katika
Riwaya hii ameleta fujo zake kama vile umalaya, mauaji na mengine mengi
na baadae kutoweka.
Yaliyomo
·
2Muundo
·
3Msuko
·
4Mtindo
Fani za kijadi ni zilisababisha Riwaya
izalike. Katika riwaya hii ya Dunia ni uwanja wa fujo” ni mojawapo ya riwaya
iliyotokana na fani za kijadi ambayo ni sira, Sira ni fani ya kijadi ambayo
hujumuisha wasifu na tawasifu yaani habari za maisha ya watu kwa mfano
mwandishi E. Kezilahabi katika riwaya yake hii imejaribu kumuonyesha mhusika
Tumaini maisha aliyokukuwa akiishi
Mfano uk. 11, “Alibatizwa , alikuwa mtoto
wa mwalimu Kapinga……”.Vile vile Tumaini alikuwa mlevi, Malaya, mfano uk. 73
“mwenyewe kaingiaaaa, tajiri wetuuu” Hivyo basi riwaya hii inasadifu kuwa ni
moja wapo kuwa ni riwaya ya fani za kijadi ambayo hujumuisha wasifu wa mhusika
Tumaini toka mwanzo wa maisha yake hadi m wiho wa maisha yake.
Muundo ni namna visa na matukio hufuatana
kwa mtiririko. Hivyo tunaweza kusema pia muundo ni mfuatano wa masimulizi
katika kazi ya fasihi. Katika riwaya hii ya “Dunia ni uwanja wa fujo”mwandishi
ametumia muundo wa rejea pamoja na changamano. Katika muundo wa rejea mwandishi
anaanza kwa kuonyesha maisha ya Dennis pale aliipowapokea wageni akina Tumaini
na pia kulejelea kwa kuonyesha maisha dennis pale tangu utoto wake, (uk.66).
Pia mwandishi ametumia muundo wa muundo
changamano au rukia ambapo visa vinakuwa vinarukiana hii inajidhihilisha sehemu
ya kwanza ambapo mwandishi anatuonyesha nyumbani kwa kasala ambaye anaishi
kijijini Bugolola kisa hakijaisha tunaona mwandishi pia anatuonyesha kisa cha
tumaini katika (uk.11):ambapo mwandishi anaonyesha kuzaliwa na kubatizwa kwa
Tumaini.
Mwandishi wa riwaya hii pia ameigawa kazi
yake katika sehemu kuu tatu na katika kila sehemu amezipa namba ili kusadifu
yaliyomo katika kazi yake ya riwaya.
Sehemu ya kwanza; Katika sehemu ya kwanza
mwandiskhi E. Kezilahabi amewachora wahusika kwa kuonyesha adha na matatizo
mbalimbali yanayoikabili jamii ya Bugolola kwa mfano ushirikina, umalaya, na
elevi mambo hayo yote ameyaonyesha katika (namba 1,2,3,4,5). Sehemu ya pili;
Pia katika sehemu ya pili tunamuona tumaini akiwashawishi akina john na
anastasia kwenda nao mjini Dae es salaam, lakini inakomea Shinyanga baada ya
dada ya kukutana na Dennis kitu kitu kilichompelekea Tumaini na wenziwe kuanza
maisha mapya mjini shinyanga. Lakini katika maisha hayo Tumaini na John
wanakuwa ni wenye kupenda Pombe na ansa kitu kilichopelekea kufilisika kwa
Tumaini. Sehemu ya tatu; inaonyesha baada ya tumaini kuamua kufanya kazi na
kupata mafanikio makubwa , lakini mafanikio hayo yanaingio doa baada ya
serikali kuingiza mfumo wa ujamaa kitu kilichopelekea mali zote za tumaini.
Mwisho kabisa tunamuona Tumaini akichukua jukumu la kumuua mkuu wa wilaya ya
shinyanga ambaye ndiye alikuwa msimamizi mkuu wa shughuli za ujamaa, kitendo
hicho kinapelekea hukumu ya kifo ka Tumaini. { namba 12,13,14}
Mbunda Msokile (1992:206) anasema kuwa
msuko ni mtiririko au mfuatano wa matukio yanayosimuliwa kuanzia mwanzo mpaka
mwisho. Hali hii huandamana na uchaguzi au mpangilio na ufundi wa kusimulia
matukio yaliyoungwa vyema katika kazi ya sanaa ya kubuni itumiayo lugha. Lakini
si tofauti na ule ufafanuzi huu si tofauti na ule unaofafanua muundo, kwani nao
ni mtiririko wa matukio jinsi jinsi yanavyopangwa kiufundi kutoka mwanzo wa
simulizi hadi mwisho.
Pesa za urithi alizoachiwa Tuamini pamoja
na malezi mabaya kutoka kwa wazazi wake ndio zinakuwa usababishi wa utonvu wa
nidhamu wa Tumaini katika kijiji chao cha Bugolola, mambo hayo ya uonvu wa
nidhamu ni kama vile;- mlevi, Malaya, kutofanya kazi, pia alitumia ovyo mali
alizoachiwa. Mfano katika (uk.15) “tunamuona mama yake Tumaini akimkabithi
Tumaini funguo ya kufungua sanduku la marehemu baba yake ammbalo lilikuwa
limebeba urithi wake.
Tumaini baada ya kupewa pesa za urithi hapa
ndio tunaona mshitikizo kwani kwani pesa za urihi zilimsababisha kuamua kuacha
shule na kuanza kuzitumia pea hizo ovyo kama vile ukahaba umalaya, ulevi, na
mengineyo. (Uk. 16, 17).
Pia katika riwaya hii msuko unaendea
kuonekana pale ambapo Tumaini, John, na Anastazia walipofika Mwanza na kufanya
maamuzi ya kuelekea Daes saalam baada ya kuona eneo la Mwanza haitawafaa kwa
kuanza maisha mapya kwani palikuwa karibu mno na kijini kwao, sababu nyingine
ilikuwa Akina Tumaini hawahuondoka kijijini kwao kwa wema. Safari yao ya
kuelekea Dar es saalam inafikia kikomo pale ambapo walipofika Shinyanga na
kukutana na Dennis ambaye aliwasihi wasitishe safali yao ili aambatane nao
wakapajue kwake na kumpasha habari juu ya mambo yaliyokuwa yakiendelea kijijini
kwao Mugele (uk.55-72).
Hali ya kuahilisha safari ya kuelekea
Shinyanga ilisababisha akina Tumaini kuanza maisha mapya mjini Shinyanga na kwa
vile Tumaini alikuwa na pesa nyingi za urithi alianza maisha ya anasa hali hiyo
ilipelekea kuishiwa Tumaini kipato na kumpelekea Tumaini kutafuta kazi ya
ulinzi ambayo alisaidiwa na Dennis katika kuipata ajija hiyo(uk.114). Lakini
pindi alipoanza kazi hiyo alijikuta akichukiawa na watu mbalimbali kutokana na
kazi yake ya kuchunguza watu sili zao na kuzilipotisha serikarini. Kzi hiyo
ilisababisha hata baadhi ya watu kumkimbia Tumaini mahali alipotia mguu wake.
Mfano pindi alipofika baa wateteja walikunjwa haraka haraka na kukimbia hali
hiyo ilisababisha wenye biashara zao kumchukia Tumaini na ikafikia hatua ya
kumtafutia Tumaini wajambazi wa kumuadabisha Tumaini.
Baada ya Tumaini kutafutiwa majambazi na
kuwa ameadabishwa hali hiyo inatumika kama usababishi wa Tumaini kuichukia kazi
yake na kuamua kutafuta kazi nyingine ya kujiajili yeye mwenyewe, kazi yenyewe
ilikuwa ni kazi ya ukulima japo alianza kama mkulima mdogo lakini baadae
akajikuta akipata maendeleo makubwa katika kazi yake mfano alinunua shamba
kubwa na alitumia Trekta katika shuguli zake za kilimo. lakini ngombe wa
maskini hazai serikali ikapitisha mfumo wa ujamaa ambapo ilidai hakuna umiliki
binafsi na mali zote ni za ni za umma hali hiyo ilisababisha kumuingiza tumaini
matatani kwa hakukubaliana na hali hiyo na kupelekea kufanya tukio la mauaji
ambapo alimuua mkuu wa wilaya ambaye ndiye alikuwa ni kiongozi wa ujamaa
(uk.114) , Kitendo hicho kilitumika kama usababishi kwa Tumaini kuwekwa chini
ulinzi wa polisi na hatimaye kuhukumiwa kunyongwa (Uk.131).
No comments:
Post a Comment