Mtindo ni jinsi msanii anavyotumia ufundi,
umahiri na hisia zake katika kutenda au kueleza jambo fulani. katika riyawa hii
kuna mitindo mbalimbali ambayo mwandishi ameitumia ni kama vile;
VIPENGELE VYA MTINDO VILIVYOTUMIKA KATIKA
RIWAYA HII; Monolojia [Masimulizi] kwa kiasi kikubwa mwandishi ametumia lugha
ya masimulizi katika kuelezea visa/matukio, sifa na tabia za wahusika katika
kuikamilisha kazi yake.
mtindo wa Barua, mwandishi pia ametumia
mtindo wa barua, m kwa mfano katika uk.68 mwandishi ametumia mtindo wa barua
tunaona Vera akimwandikia Denis barua, pia uk.105 mwandishi ametumia mtindo huu
wa barua , Tunamuona Tumaini akimuandikia Joku barua vilevile katika uk.110
“tunamuona Denis akipokea barua kutoka kwa Vera”, uk.123 “bibi Kimalio alimuandikia barua denis”.
Hotuba, mwandishi katika kazi yake hii ya
riwaya ya “Dunia ni uwanja wa fujo” ametumia mtindo wa hotuba. Kwa mfano katika
uk. (115 - 117) mtindo wa hotuba umetumika na hotuba ilikuwa ya kusisitiza
Azimio la Arusha ambalo lililenga hatua ya siasa ya ujamaa nakujitegemea ambayo
ilitaka watu wote wamiliki mali na uchumi kwa pamoja bila kujali mwenye nacho
na asiye ncho.
Nyimbo; ni mtindo mmoja wapo aliotumia
mwandishi aliotumia mwandishi wa riwa hii. Kwa mfano uk.10 mwandishi ametumia
wimbo ulioimbwa na mpiga zeze.
“Wanaume Bugolola
Mchana hawajambo
Usiku hawana tendo”
Mwandishi pia ametumia wimbo kwa mtindo wa
shairi katika kazi yake hii kwa mfano katika uk.13 tunona Tumaini akiandika
shairi ambalo lilisomwa na mwalimu darasani kama ifuatavyo.
“Yeh,
Nitaoa msichana
Msichana mwenye shingo
Shingo shingo kama la
mbuni..”
Mwandishi E. Kezilahabi ametumia wimbo wa
maungunzo, mwandishi katika mtindo wa mazungumzo ametumia nafsi zote tatu yaani
nafsi ya nafsi ya kwanza, nafsi ya pili, nafsi ya tatu katika kazi yake yake
hii ya Dunia uwanja wa fujo”
kwa
mfano.
- Uk. 13 tuaona nafsi ya kwanza umoja
“nitaoa msichana” na
- uk.27 tunaona nafsi ya kwanza wingi. “hata sisi,” pia
- Pia nafsi ya pili katika riwaya hii
imetumika kwa mfano uk.36 “…wewe kasala Pia nafsi ya tatu katika riwaya hii
tunaona katika uk.35 “….yeye alisema kwa machozi
MATUMIZI YA LUGHA Lugha ni muhimu katika
kazi ya fasihi. Posipo lugha hakuna riwaya. Mwandishi wa riwaya hii “Dunia ni
uwanja wa fujo” ametumia lugha sanifu iliyosheheni taswira, mkoto, misemo,
methali, tamathali za semi, nahau, lugha za kigeni, na mbinu zingine, za
kisanaa kama ifuatavyo:- Lugha sanifu ni moja wapo ya ambayo mwandishi ametumia
toka mwanzo hadi mwisho. Lugha iliyotumika ni Kiswahili sanifu. Pia mwandishi
ametumia lugha isiyo sanifu kwa kiasi kidogo. Kwa mfano katika uk. 5, Mwandishi
anasema “…. Batoto bamenisosondogorasondogola na chichwa, bengine
bamenikorokorakorokora na kucha”. Uk. 30 “…. Vizuri walilia kwa sauti za kutisha,
yuhuu. Huba, huba, huba. Wotha ,wotha”
Luha ya kigeni; imetumiwa na mwandishi E. Kezilahabi katika riwaya yake hii. Lugha ya kigeni aliyotumia ni kiingeleza kwa mfano:-
- “Africans royal bar” (uk. 62).
- “Snow cap” (uk.62) - “You are too
optimistic about life and you are too pessimistic” (uk.65, 66). - “Welcome
back” (uk.88). - “Security (uk.89 na 90).
Mchanganyo ndimi; ni matumizi ya lugha
ambayo mwandishi ametumia katika riwaya hii. Mchanganyo ndimu ni ile hali mtu
kuongea kwa kutumia lugha zaidi ya mbili. - Mfano. (Uk. 41) “mimi …naturalist”.
lugha za matusi; Ni Mbinu nyingine
ilizotumiwa na mwandishi katika riwaya hii ni lugha za matusi kwa mfano. -
“Washenzini ninyi”.(uk.12). - “Kumbe bado washenzi” (uk.50). - “Yule mshenzi
amekwenda” (uk.93) - “Nimemfukuza mbwa tumaini (uk.109). - “Kwanza wewe bwege.
(uk.121). -“…. Alidakia na kusema unyokonyoko (uk.122).
Tamathali za semi; ni maneno yanayotumiwa
yanayotumiwa na wasanii Ili kutia nguvu katika kazi hiyo. Hivyo tamathali za
semi zinazotumika katika riwaya hii ni pamoja na Tashibiha/Mshabaha. Ni maneno
ambayo hutumia kulinganisha kitu na kitu na kitu kingine kwa kutumia maneno
kama vile “mithili, sawa, kama” mfano:- - “Miaka ni kama kunguni” (uk.6). -
“Baba yako atakuwa mkali kama samba” (uk.6). - “Mapenzi ni kama mpunga mototo
wangu” (uk.14). - “Lakini mimi ninaumwa ninaumwa kama panya.” (uk.17). - “Si
tutakufa kama mbwa”. (uk.19). - “Kukaa kama watakatifu”. (uk.19.) -
“Aliyekunyata nyumbani kwake kwa uoga kama panya aliyesikia mlio wa paka”.
(uk.130).
SITIARI Ni tamathali za semi ambazo
ulinganisha vitu vizuri kwa kutumia viunganishi au linganishi.mfano “ni”:- -
“Watoto wote yatima ni watoto wangu”. (uk.15). - “Huyo ni baba yako” (uk.12). -
“Ujamaa ni mzuri”. (uk.112). Takriri ni tamathali za semi ambayo neon
hujirudiarudia kwa lengo la kusisitiza jambo Fulani. Takriri ni matumizi ya
lugha ambayo msanii ametumia katika riwaya hii, mfano wa takriri:- - “Mauti,
mauti”. (uk.17). - “He! Hee! Hee!” (uk.18) - “Kasala, kasala, ngoja
nije !”(uk.22) - “Yuhu! Yuhu!” (uk.27) - “Haa! Haa! Haa! (uk.42) - “Msiue,
msiue!” (uk.44)
Tashihisi; Ni tamathali za semi ambazo vitu
ambavyo si viumbe hai hupewa hadhi ya kutenda kama binadamu. Mfano:- - “Mwezi
uliona nyota ziliona hata jua liliona.” (uk.12) - “Tumaini alisikia sauti kama
ya ndege akiimba kwa huzuni.” (uk.19) - “kila jiwe walilokalia liliwaambia
“samahani umekalia bega langu”. (uk.32)
Anakali sauti. Ni tamathali ya semi ambayo
uigaji wa sauti za asili. Mfano Katika riwaya hii tanakari sauti alizotumia
msanii ni kama ifuatavyo:- “boooouuu! (uk.130)
Tafsida, - “Kazi kutembeza kengele zako
kwenye mabaa.” Uk.121. - “Tumaini alikuwa akishika mahali pabaya”. Uk.53.
Tashihisi, ni Tamathari hii hufanya vitu ambavyo havina uhai wa kutenda jambo kama binadamu vitende au vifanye jambo hilo kama binadamu, mfano wa tashihisi zinazojitokeza katika riwaya hii ni:mfano:- - “Mwezi uliona nyota ziliona hata jua liliona.” (Uk.12) - “Tumaini alisikia sauti kama ya ndege akiimba kwa huzuni.” (Uk.19) - “Samaki amejileta mwenyewe ndani ya chungu.” (Uk.19) - “Kila jiwe walilokalia liliwambia samahani umenikalia bega langu.” (uk.32)
Methali Usemi wa kisanii wa kimapokea
unaofikiriwa na jamii kuwa kweli na unaotumiwa kufumbia au kutolea mifano na
huwa unabeba maana pana kuliko maneno yenyewe yanayotumiwa. Kwa mfano:- - “Wema
wa mtu hujulikana siku ya mazishi yake.” (Uk.13) - “Ugonjwa haufichwi. Afichae
ugonjwa ndio hufa.” (Uk.29) - “Kweli wajinga ndio waalimu wa kuwafunza welevu.
(uk.78) - “Ukishikwa shikamana.” (Uk.102)
Misemo Ni mafungu ya maneno yanayotumiwa na
jamii ya watu wa lugha hiyo kwa namna maalumu ili kutoa mafunzo, maadili na
kuihadharisha jamii. Misemo ni maneno ambayo jamii huyatumia kutokana na uzoefu
katika maisha. Kwa mfano: - “Ponda mali kifo chaja.” (Uk.10) - “Ulimwengu hauna
mwema.” (Uk.103) - “Mapenzi yao sasa yalikuwa yamekwisha pata kovu”. (Uk.108) -
“Nilitaka uniondoe kwenye mdomo wa samba.” (Uk.24)
Nahau Haya ni mafungu ya maneno yenye maana
maalumu ambayo haitokani na maneno ya kawaida yaliyopo kwenye maneno hayo.
Nahau za lugha yoyote hutumiwa zaidi na jamii yenye asili ya lugha hiyo. Kwa
mfano:- - “Amezunguka mbuyu - amekula rushwa”. (uk.25 -“Unamvika kilemba cha
ukoko”. (Uk.71) Tanakali sauti - “Booouuu!”
Mjalizo, Katika tamathali hii sentensi huwa ni mfuatano tu wa maneno yasiyo na viungo vyovyote. Mfano:- - “Wenye mashoka ! wenye mikuki na miundu! Wenye pinde na wenye mapanga walianza kulifyeka lile chaka”. (Uk.27)
Lugha ya matusi. - “Nimemfukuza mbwa , tumaini!” (Uk.109) - “Unakili … Mama bahati alisema nyokonyoko”. (Uk.122) - “Piga mbwa watu wa huku washenzi “(uk.50) Halima alizoea kuwatukana washenzi nyinyi. (uk.12)
Lugha ya picha. - “Kipofu kipofu! Washa taa
uone vizuri.” (uk 10) - “ukioa msichana mzuri hata ndege watakuwa wanatua juu
ya vichwa vyenu”. (uk.15) - “Alikuwa ameoza nje na ndani”. (Uk.53) - “Lakini
sasa ninaamini kuwa dunia ni uwanja wa fujo”. - “Ukioa mwenye tabia mbaya mchwa
watajenga vichuguu ndani ya nyumba yenu”. Uk.15
WAHUSIKA
Wahusika ni watu au viumbe waliokusudiwa
wawakilishe tabia za watu katika kazi za fasihi. Wahusika wa fasihi ni wa aina
kuu tatu,wahusika kazi ya fasihi wanaweza kuwa wahusika wakuu, wahusika wadigo,
na ewahusika wajenzi.Wahusika huonyesha dhana mbili muhimu katika maisha ya
watu yaani wema na mabaya pia wahusika humaanisha tabia maalumu iliyokusudiwa
na jamii. Katika riwaya ya “Dunia uwanja Fujo” wahusika wake ni mhusika mkuu,
whusika wadogo, na wahusika wajenzi kama alivyoainisha Catherine Ndugo (1991)
na Wangali Mwai(1991).ika riwaya hii mwandishi ametumia wahusika wa aina tatu
kwa kutumia kigezo cha Catherine na Wangeri Mwai(1991) Kama wahusika wakuu,
wadogo, na wajenzi kama ifuatavyo:-
MHUSIKA MKUU Mhusika mkuu; huyu ni yule anejitokeza kila mara katika kazi za fasihi tangu mwanzo hadi mwisho. Maudui ya kazi ya fasihi huwa yanamzungukia na hata kutolewa na mhusika mkuu zaidi ya wahusika wengine.
TUMAINI. Huyu Ndio mhusika mkuu katika
riwaya hii kwani maudhui na dhamira zimejengwa juu yake. Pia tunaona wahusika
wajenzi akina John, Anastazia, Dc, na mgeni kutoka Dar es saalam dhamira
wanazozitenda zinamgusia mhusika mkuu ambaye ni Tumaini. Jina Tumaini ni jina
ambalo amepewa na mzazi wake mzee Kapinga ambaye alikuwa mwalimu. Jina Tumaini
linasadifu matumaini ya wazazi wake, pia alikuwa ni mototo pekee wa kiume
katika familia ya mwalimu Kapinga pia walikuwa na matumaini pindi atakapomaliza
shule ndio atakuwa msaada wao katika familia na pindi watakapokuwa
wazeeka.mambo hayo yanapatikana katika (uk.11). inasema “… Naam Tumaini alikuwa
motto wa watu hawa. Tumaini kama jina lenyewe lionyeshavyo alikukuwa peke yake
katika tumbo la mama yake…..”
WASIFU WA TUMAINI - Alikuwa ni motto wa
Kapinga. (uk.9) - Alikuwa Malaya (uk.8, 24) - Alikuwa mlevi (uk.94) - Mchapa
kazi (uk. 114) - Mtumia Pesa vibaya (uk. 55) - Alikuwa muuaji. (uk.128) -
Alikuwa na mapenzi ya dhati kwa mkewe (uk.128) Alikuwa na matusi (uk. 12)
WAHUSIKA WADOGO WADOGO
Hawa
ni wahusika ambao hawajitokezi mara kwa mara katika kazi ya fasihi ndio ambao
husimamia dhamira ndogo ndogo Katika
riwaya hii ya “Dunia uwanja wa fujo” wahusika wadogo wadogo waliojitokeza ni
kama ifuatavyo:-
1. KAPINGA.
SIFA ZA KAPINGA
- Baba yake na Tumini. (uk.9) - Alikuwa
mwalimu. (uk.9) - Alikuwa na malezi mabaya kwa mwanae. (uk.12) - Alikuwa ni
Mume wa miango. (uk.9) - Alikuwa ni mbinafsi. (uk.15) - Alikuwa hapendi
kushilikiana katika jamii. (uk. 12).
2. KASALA
SIFA
ZA KASALA
- Ni mwanakijiji wa Bugolola. (uk. 1). -
Mtoto wa Mugala. (uk. 2). - Baba yake na Misana. (uk. 2). - Mume wake na
Mugele. (uk. 2). - Mtu mwema. (uk. 4). - Kiasi Fulani alikuwa ni mvivu .(uk.6)
3. MUNGERE
SIFA ZA MUNGERE;-
- Mke wa Kasala (uk.2). - Mama yake na
Misana (uk.2). - Mwanakijiji wa Bugolola (uk.2). - Mtu mwema na mchapa kazi .
(uk. 4).
4. MISANA.
SIFA MISANA;-
- Mtoto wa Kasala (uk.2). - Alikuwa mtundu.
(uk.3). - Mtoto wa Mungere (uk.2). - Mdogo wao na akina Dennis, Leonila,
Aulelia. (Uk.5). 5. MUGALA - mwananchi wa Bugolola. Uk.3 - Mchawi. Uk.3 na 7. -
Ni mama yake na Kasala. uk.2 - Ni mjane uk.4. - Mtu mwenye hasila uk.22 -
Alikuwa na malezi mabaya kwa wajukuu zake uk.19 6. LEONILA - Alikuwa dada yake
Dennis na Misana . - Alikuwa ni motto wa Kasala Mungere. - Alikuwa ni mpenzi wa
Tumaini uk. 8 na 24. 6. BENADETA - Mke wa pili wa Dennis uk. 121 - Mtu mwenye
chuki uk. 120 - Alikuwa na dharau na mwenye matusi. uk 121
7. CHRISTINA - Alikuwa kahaba. Uk.96 - Alikuwa mlevi uk.94 - Alikuwa mlagai uk.95 - Hana mapenzi ya dhati uk.96 - Alikuwa anapenda sana pesa. Uk. 94
8. MAKOROBOI - Alikuwa jambazi uk.96 -
Alikuwa mkatil na mwenye kisasi uk.96 - Anapenda pesa. Uk.96
WAHUSIKA WAJENZI Ni wahusika ambao maudhui
yao na dhamira wanazozitenda zinamsaidia mhusika mkuu katika dhamira
azitendazo. Mara nyingi wahusika wajenzi wanakazi ya kunjenga au kumsaidia
mhusika mkuu katika dhamira zake. Katika riwaya hii wahusika wajenzi ni kama
ifuatavyo:- 1. JOHN JOHN Ni mhusika mjenzi kwani dhamira alizobeba na nafasi
alizotumiwa na mwandishi ni kwa lengo la kumjenga mhusika mkuu tumaini. Pia
tunaona John na Tumaini walikuwa na mahusiano na ushirikiano tangu wakiwa kijijini
Bugolola mpaka waliposafiri kuelekea mjini Shinyanga. -Alikuwa mlevi uk.62
-Alikuwa Malaya uk.62 na 66. -Alikuwa mvivu uk. -Anamapenzi ya dhati uk.97
2. ANASTAZIA Anastazia pia huyu ni mhusika mjenzi kwani alikubali kuambatana na Tumaini kijijini kwenda Mwanza halafu mjini Arusha. Pia uhusiano wao ulidumu na kupelekea kuoana na Tumaini.
WASIFU WA ANASTAZIA NI KAMA IFUATAVYO:- -
Alikuwa na mapenzi ya dhati. Uk.57, 97, & 99. - Alikuwa mke wa Tumaini. Uk.
61 - Mtu mwenye huruma uk.99 - Mtu mvumilivu. Uk.89
3. DENNIS Ni mmoja wapo wa
wahusika wajenzi kwani ndio anaemjenga mhusika Tumaini kwa kiasi kikubwa akiwa
mjini Shinyanga. Pia TUMAINI ALIKUWA NA SIFA ZIFUATAZO -Ni mtu mwenye mapenzi
ya dhati. Uk.59 -Alikuwa ni mototo wa Kasala. Uk 3 - Alikuwa ni mtumishi wa
serikarini
No comments:
Post a Comment