MAUDHUI
Maudhui katika kazi ya fasihi ni jumla ya
mawazo yote yanayozungumzwa pamoja na mtazamo wa mwandishi juu ya mawazo hayo.
Maudhui hujumuisha mawazo pamoja na mafunzo mbalimbali yaliyomsukuma msanii
hadi akatunga na kusanii kazi fulani ya kifasihi. Vipengele vya maudhui ni
pamoja na dhamira, migogoro, falsafa ujumbe na msimamo.
Katika riwaya hii Dunia uwanja wa fujo
mwandishi amejitahidi kwa kiasi kikubwa kuonyesha maudhi mbalimbali katika kazi
yake kupitia vipengel;e mbalimbali kama vile Dhamira, migogoro, ujumbe,
falsafa, mtazamo itikadi hii yote ni kwa lengo kuu la la kuelimisha jamii
kuhusu mambo mbalimbali yanayotukia katika jamii hiyo.
Dhamira; hili ni wazo kuu au
mawazo mbalimbali yanayojitokeza katika kazi ya fasihi. Senkoro anataadharisha
maana hii isichanganywe na maudhui kwani dhamira ni sehemu tu ya maudhui na
aghalabu dhamira kuu ndio hujenga kiini cha kazi ya fasihi. Dhamira
zimegawanyika katika makundi mawili, kuna dhamira kuu na dhamira ndogondogo.
Dhamira kuu ni wazo
kuu linalojitokeza katika kazi ya fasihi, dhamira kuu katika riwaya
hii ni matatizo na mikinzano ya kijamii, kiuchumi, na kisiasa, sasa tuangalie
ni kwa jinsi gani mwandishi ameijadili dhamira hii;
Matatizo na mikinzano ya kijamii, kiuchumi,
na kisiasa, Katika riwaya hii “Dunia uwanja wa fujo” kwa kiasi kikubwa riwaya
hii imejikita katika dhamira hii ambapo ameonyesha matatizo na mikinzano
kiuchumi na kijamii ambayo jamii ya kitanzania iliyoandikiwa hukabiliwa nayo.
Ili kuijenga dhamira hii mwandishi amewatumia wahusika kama vile Tumaini, John
,Anastazia, Kapinga, Dennis ili kuiunda dhamira yake kuu katika riwaya hii.
Tukianza na Tumaini mwandishi amemuonyesha kuwa ni mhusika ambaye anapinga sera
za kijamaa ya siasa ya ujamaa iliyoanzishwa na serikari nchi nzima hali hiyo
inaleta ukinzani kwa tabaka lenye mali kwani hawakuwa tayari kuachia mali zao
kwa umma. Hali hii inadhihilisha pale Tumaini alipoamua kupingana na hali hiyo
ya kunyanganywa mali zake na kupelekea kumuua mkuu wa wilaya, ambaye alikuwa
ndio kiongozi mkuu katika mkoa Shinyanga katika shughuli za kusimamia sera hiyo
ya ujamaa.(uk.127) Hali hiyo ni mfano tosha kudhihilisha kuwa dhamira
kuu katika riwaya hii ni Matatizo na mikinzano ya kijamii, kiuchumi, na
kisiasa.
Dhamira ndogo ndogo.Haya ni mawazo
yanayojitokeza ili kujenga dhamira kuu. Dhamira ndogondogo zinazojitokeza
katika riwaya hii ni;
MAPENZI NA NDOA.
Mwandishi E. Kezilahabi amejadili suala la
mapenzi na ndoa katika pande mbili tofauti, kwanza ameonesha mapenzi ya dhati
na mapenzi ya ulaghai lakini pia ameonesha ndoa za dhati na ndoa za ulaghai.
tukianza na mapenzi ya dhati, mapenzi ya dhati yanajitokeza kwa:
a) MAPENZI YA DHATI
KWA TUMAINI NA MKEWE ANASTAZIA
Mwandishi ameonesha mapenzi ya dhati
aliyokuwa nayo Tumaini kwa mke wake, Mwandishi anathibisha hili pale anapoamua
kutoroka na Anstazia na kuelekea mjini Shinyanga ambako walianza maisha mapya
pia tunaona jinsi gani wawili hawa walivyojaliana hata katika kipindi cha
matatizo. Mfano Anastazia alionyesha mapenzi ya kweli pale alipompelekea
Tumaini chakula na kumfaliji kuwa atapona, pindi Tumaini alipopigwa na akina
makoloboi. Uk.97
Mapenzi ya dhati aliyokuwa nayo kwa mke
wake pia yanajidhihirisha pindi mke wake huyo alipokubali kuishi na Tumaini
japo alikuwa ni mhuni na mlevi pia ha baada ya Tumaini kupigwa na kualibiwa
sura Anastazia alindelea kuafiki kuishi na na Mumewe Tumini, hii ni kwa kuwa
alikuwa akimpenda. Mwandishi anathibitisha hili katika. [Uk 64]
2. Ulevi.
Mwandishi E, Kezilahabi hakuwa nyuma
kujadili suala la ulevi na athari zake kwa binadamu na jamii kwa ujumla, katika
riwaya yake hii amemtumia muhusika Tumaini pamoja na John kuelezea
dhamira hii. Tukianza na Tumaini, mwandishi anamwonesha Tumaini akianza tabia
ya ulevi wa pombe kali baada ya kufiwa na wazazi wake kijijini Bugololola hata
alipoamia mkoani Shinyanga aliendelea na tabia hiyo ya ulevi wa pombe,
Mwandishi hakuishia hapo tu bali ameonesha na athari za tabia hiyo ya ulevi
kama vile kupelekea kufilisika kwa tumaini kama mwandishi
anavyothibitisha (Uk 94 &95)
3. MALEZI KWA WATOTO.
Hii ni dhamira nyingine inayojitokeza
katika riwaya hii, Mwandishi amemtumia muhusika Tumaini kuilezea dhamira hii,
tunamwona Tumaini akipata malezi mabaya kutoka kwa wazazi wake kitu
kilichopelekea kuyahalibu maisha ya Tumaini na kumfanya aache shule, awe mlevi,
pamija na mengine mengi.
Mfano Siku moja Tumaini alimchoma mlezi
wake jichoni. Yule kijana alimpiga Tumaini kidogo, Tumaini alikimbia kwenda
kushtaki kwa mama yake. “Mama Mpishi amenipiga!” Kwa nini
umempiga mtoto wangu !” Mugaya alifoka.” Hali hii inaeleza jinsi Tumaini
alivyo lelewa vibaya na kudekezwa na wazazi wake; uk 11
USHIRIKINA NA UCHAWI
Ni hali ya kuamini nguvu za giza, ni jambo
ambalo lina sababisha jamii nyingi kugawanyika na kukosa amani. Kwani
mwandishi anadhihirisha hili anaposema;
“Vizuu walilia kwa sauti ya
kutisha : yuhu!yuu! huba!”uk. 30.
“Tena alikuwa akilala ndani ya nyumba yako! Ndio
maana mama yako alikuwa mchawi”uk. 36.
Suala la ushirikina katika jamii
inayotuzunguka ni janga ambalo kila siku linahatarisha maisha ya watu hususani
wazee wenye macho mekundu wako hatiani kupoteza maisha yao katika baadhi ya
maeneo mfano mkoa wa Shinyanga na Simiu,hivyo dhamira hii haijapitwa na wakati.
UNAFIKI.
Hii ni dhamira pia inayojitokeza katika
riwaya hii, katika kuijadili dhamira hii Mwandishi amemtumia mke wa
Dennis kama mtu mnafiki kwani alijifanya anampenda mmewe kumbe alikuwa na
uhusia mwamume mwingine ambaye ni John rafiki y yake na Dennis.
Mwandishi anadhihilisha hali hiyo akionyesha katika kitabu chake kwamba;
“Heshima yangu imekwishapotea John ukiniacha hivihivi
nitaona aibu sana!”uk72.
Tukigeukia katika uhalisia, tabia hii ya
unafiki imeshamiri katika jamii zetu, unaweza ukawa na rafiki au ndugu ambaye
akawa mnafiki kwako. Jamii inatakiwa kuondokana na tabia hii kwa haifai kabisa.
NAFASI YA MWANAMKE.
Katika riwaya hii mwanamke amechorwa katika
pande mbili, amechorwa katika upande hasi lakini pia mwanamke amechorwa katika
upande chanya, upande hasi mwanamke amechorwa kama kiumbe duni na dhaifu wakati
katika upande chanya amechorwa kama mtu jasiri, mchapa kazi, mwenye upendo.
n.k. Sasa hebu tuangalie nafasi ya mwanamke katika jamii kama alivyochorwa
katika riwaya hii tukianza na upande hasi;
Katika riwaya hii mwanamke amechorwa kama
kiumbe duni, dhaifu, katika nafasi mwanamke amechorwa kama;
A) CHOMBO CHA STAREHE.
Mwandishi amemchora mwanamke kama chombo
cha starehe anayeweza kutumiwa kuwastarehesha wanaume ili mradi kufurahisha
nafsi zao, hili linathibitishwa na Mwandishi katika riwaya hii akimtumia
muhusika Christina kama chombo cha starehe, ambaye alionekana kujirahisishwa
kwa wanaume ili mladi apate fedha. Mfano;uk 95 & 96.
“Sijaona mwanaume mwoga kama wewe!
Kristina alisema.
Tumaini alilala
kitandani. Kristina alizima taa”uk.96
Hata katika jamii yetu inayotuzunguka
wanawake kwa kujijua au kutojua wamekuwa wakifanywa kama chombo cha starehe
kuwastarehesha wanaume, jamii inatakiwa kubadilika na kuondokana na dhana hii
kwani mwanamke pia anastahiri heshima katika jamii.
B) MTU ASIYE NA MAAMUZI KATIKA JAMII
Mwandishi amemchora mwanamke kama mtu asiye
na maamuzi katika jamii yake, kwa mfano anamtumia muhusika ambaye alikuwa nini
mama yake Tumaini kushindwa kufanya maamuzi juu mali alizoziacha kama urithi wa
Tumaini japo hakupenda kumuachia mtoto wao fedha nyingi(alijua zitamuangamiza
mwanae) lakini alishindwa kubatilisha kutokana na maamuzi yaliyoachwa na
mumewe.mfano anaonyesha;
“Ni vizuri zaidi mtoto kurithi vitu kama hivyo, licha
ya hekima na kumrithisha mototo pesa ni ni kunvisha taji la uovu.” Baba yako
alikataa kabisa; na kwa kuwa nilishindwa mawazo ya baba yako alipokuwa
bado mzima, siwezi sasa kugeuza tamshi lake.” uk15
Hata katika jamii yetu, inawachukulia
wanawake kama watu wasio na maamuzi katika familia na pindi inapotokea kufiwa
na waume zao huwa wanapata shida na manyanyaso kutoka kwa ndugu wa mwanaume
kama vile kufukuzwa kwenye nyumba, kunyang'anywa watoto na mali nyingine
alizoshirikiana kuzichuma na mumewe. jamii inatakiwa kumpa nafasi mwanamke na
itambue kuwa ana haki sawa kama mwanaume.
MWANAMKE AMECHORWA KAMA MSALITI.
Hii ni nafasi nyingine ambayo mwandishi
amemchora mwanamke, kwa mfano tunaona mke wa Dennis kama mtu mnafiki kwani
alijifanya anampenda mmewe kumbe alikuwa na uhusia mwamume mwingine
ambaye ni John rafiki y yake na Dennis. Mwandishi anadhihilisha hali hiyo
akionyesha katika kitabu chake kwamba;
“Heshima yangu imekwishapotea John ukiniacha hivihivi
nitaona aibu sana!”uk72.
Migogoro; ni mivutano na
misuguano mbalimbali katika kazi za fasihi. Migogoro inaweza kuwa kati ya
wahusika, familia zao, matabaka yao, au hata katika nyadhifa mbalimbali.
Vilevile migogoro yaweza kuwa ya kiuchumi,
kijamii, mogogoro ya nafsi, na migogoro ya kisiasa ambayo hujitokeza katika
mitazamo tofauti kulingana na mtiririko wa visa na matukio yanavyopangwa na
mwandishi. Kwa kuanza
Mgogoro wa nafsi tunamuona Tumaini akipatwa
mgogo nafsi pindi alipofiwa na wazazi wake na baadae kug unduli kuwa walikuwa
wamechuliwa ka vizuu na bibi ake na Leonila pia mgogoro nafsi wa pili ni pale
ambapo leonila ankataliwa kuolewa na Tumaini anajikuta akiingia katika lindi la
mgogoro nafsi. Pia Leonila anjikuta akiingia katika mgogo wa nafsi pindi pindi
wazazi wake walipomwandalia mazingila ya kuolewa na tembo uk.15 &39
Mgogoro kati ya mtu na mtu; Hapa tunaona mgogoro
kati ya Anastazia pamoja na wazazi wake, Dennis na John, Dennis na Benadeta,
Tumaini na Serikali,Kasala na mama yake.mfano. uk.22,23,&128.
-“Kumtunza mzee ni mzigo lakini inabibi uuchukue
kwa fulaha” uk.23
-“Baba nihurumie! Lakini
Kasala aliendelea kumpiga.
Bibi wameniua kwa sababu yako!”uk.22.
UJUMBE / MAFUNZO
Ujumbe; mwandishi anapoandika kazi yake
huwa na ujumbe ambao hutaka uifikie jamii aliyoikusudia. Ujumbe katika kazi
fasihi ni mafunzo mbalimbali ambayo hupatikana baada ya kusoma kazi ya fasihi.
Katika kazi ya fasihi dhamira kuu hubeba ujumbe wa msingi na dhamira ndogondogo
hubeba ujumbe ambao husaidia kuujenga au kuupa uzito zaidi ujumbe wa msingi.
Baadhi ya ujumbe unaopatikana katika riwaya hii ni pamoja na;-
Kikulacho kinguoni mwako, Huu ni ujumbe ama funzo
tunalolipata baada ya kusoma riwaya hii, ujumbe huu tunaupata kupitia muhusika
mama Resi pindi kwani alijifanya anampenda mmewe kumbe alikuwa na uhusia
mwamume mwingine ambaye ni John rafiki yyake na Dennis.uk.72
Majuto ni mjukuu, Ujumbe huu unajitokeza
pia katika riwaya hii, mwandishi anamtumia muhusika Tumaini pale alipoendekeza
starehe zilimsababisha aingie kwenye mtego wa majambazi wa kupigwa na
kuhalibiwa sura yake. uk.98
Elimu ni ufunguo wa maisha, Mwandishi anatupa
ujumbe mwingine kuwa, ili mtu aweze kufanikiwa hana budi kushikiria na
kuizingatia elimu kwani elimu ni ufunguo wa maisha, ujumbe huu katika riwaya
hii unajitokeza kwa muhusika Dennis ambaye alipata kazi nzuri sababu alikuwa
amekwenda shule na kupata elimu ya kutosha.
“Nyumba ya Dennis ilikuwa ni kubwa sana. Ilikuwa na
vyumba saba bila kuhesabu jiko lililokuwa mumo humo ndani” uk.60
Mpende akupendaye asiyekupenda achana nae, katika
riwaya hii anaipa ujumbe jamii yake kuwa penda pale unapopendwa na si
kumng'ang'ania tu mtu kwa kuwa moyo wako unataka tu kuwa naye, ujumbe huu
tunaupata kupitia kwa muhusika Denni alipogundua kuwa mke wake alikuwa na
mapenzi ya uongo aliamua kuachana nae.
“Dennis
alipofika nyumbani alipiga kerere nimemfukuza mbwa,Tumaini”uk.109
MSIMAMO
Msimamo; katika kazi ya fasihi, mawazo,
mafunzo na falsafa ya msanii hubainisha msimamo wake kuhusu masuala mbalimbali
ya kijamii. Msimamo ni ile hali ya mwandishi kuamua kufuata na kushikilia jambo
fulani. Jambo hili huweza kukataliwa na wengi lakini akalishikilia tu.
Msimamo ndio huweza kuwatofautisha wasanii wawili au zaidi wanaoandika
kuhusu mazingira yanayofanana. Hivyo basi mwandishi anamsimamo kwamba mambo
yote yanayotendeka katika ulingu huu ni sasawa na fujo tupu, kwani hata kama
utajitahidi vipi kupambana na shida za ulimwengu huu matatizo yataendelea
kukukabili mpaka umauti utakapokufikia.
Jina na jalada la kitabu, Tukianza na jina la
kitabu, jina la kitabu ni “Dunia uwanja wa fujo” linasadifu yale yaliyomo
ndani ya kitabu kwani tangu mwanzo wa riwaya hii kuna matukio au fujo
mbalimbali ambazo zimejitokeza fujo hizo ni kama vile umalaya, ulevi, uchawi
pamoja na mengineyo mengi. Mfano suala la uchawi lidhihilika pale katika uk.36
unasema “Tena alikuwa akilala ndani ya nyumba yako! Ndio maana mama
yako alikuwa mchawi”uk. 36.
FALSAFA YA MWANDISHI.
Kulingana na Mbunda msokile yeye anasema
kuwa Falsafa ni wazo ambalo mtu anaamimini lina ukweli Fulani unaotawala maisha
yake pamoja na maisha ya jamii. Hivyo basi katika riwaya hii anaamini kuwa
katika riwaya yake ya “Dunia ni uwanja wa fujo” Kwamba maisha hayana raha wala
maana isipokuwa dunia ni uwanja wa fuzo.
KUFAULU KWA MWANDISHI
Mwandishi wa riwaya hii amefaru kwa kiasi
kikubwa kuibua dhamira dhamira mbalimbali katika jamii. Kwani dhamira hizo
zimeonekana kuwa ni kikingamizi kikubwa cha katika maendeleo ya jamii. Mfano
suala la uchawi na ushilikina , malezi mabaya, ukale na usasa. Pia mwandishi
amefaulu katika suala zima la lugha kwani ametumia lugha lahisi na inayoeleweka
kwa msomaji yeyote hata kama si msomi mkubwa.
No comments:
Post a Comment