Thursday, April 20, 2017

Nomino (N)

Nomino ni maneno ambayo ni majinaya watu, vitu, hali n.k. Kuna nomino za kawaida na nomino za kipekee miongoni mwa aina nyingine za nomino.

Aina za Nomino

Kunazo aina mbalimbali za nomino katika lugha ya Kiswahili.
  • Nomino za Kipekee
  • Nomino za Kawaida
  • Nomino za Jamii/Makundi
  • Nomino za Kitenzi-Jina
  • Nomino za Dhahania
  • Nomino za Wingi

Nomino za Kawaida

Haya ni majina ya kawaida yanayoweza kutumiwa kurejelea vitu mbalimbali, watu, wanyama, mahali na kadhalika. Nomino hizi zinaweza kuwa katika umoja au wingi kulingana na ngeli yake.
k.m: nyumba, mbuzi, daktari, soko, kalamu, jua

Nomino za Kipekee

Haya ni majina maalum ya watu, mahali, bidhaa, kampuni, na kadhalika. Herufi ya kwanza ya nomino hizi huwa ni herufi kubwa. Nomino za kipekee haziwezi kubadilika, na hivyo basi hazina wingi.
k.m: Tanzania, Nairobi, Anita, Gafkosoft, Athi, Kimbo,

Nomino za Jamii

Nomino za jamii hurejelea kundi la vitu au wanyama, kwa ujumla. Aghalabu vitu vinavyorejelewa hutokea kwa makundi ya vitu mbili au zaidi. Nomino hizi hutumia wingi tu tunaporejelea makundi zaidi ya moja.
k.m: jozi la viatu, umati wa watu, bustani la maua, bunga la wanyama

Nomino za Wingi

Nomino hizi hurejelea vitu ambavyo hutokea kwa wingi na haziwezi kuhesabiwa. Vitu kama hivyo hutumia aina nyingine ya vipimo ili kurejelea kiasi chake. Nomino za wingi hazina umoja.
k.m: maji, maziwa, changarawe, pesa, nywele

Nomino za Vitenzi Jina

Nomino hizi huundwa kutokana na vitenzi kwa kuongeza kiungo KU mwanzoni mwa mzizi wa kitenzi.
k.m: kulima, kuongoza, kucheza, kulala

Nomino za Dhahania

Haya ni majina ya hali au vitu ambavyo havionekani wale haviwezi kushikika.
k.m: upendo, furaha, imani, elimu, ndoto, mawazo, maisha, usingizi

No comments:

Post a Comment

Inkuru nshya

Latest Fully Funded Scholarships for Undergraduates

The Major FAQs in applying or getting a scholarship is When is the Expiring?, is The Scholarship a Fully Funded Scholarship? and How Much ...